Hapa tukivuna mchumo wa kwanza.
Wednesday, February 8, 2017
Tuesday, December 6, 2016
Magonjwa ya pilipili kali
Nimeona katika pilipili nazolima zinashambuliwa sana na ukungu. Hivyo ni vyema kupuliza dawa za kukinga ugonjwa huu kama Ebony 80WP au dawa za kutibu kama tayari zimeshaathirika, dawa kama Ivory 72WP ni nzuri kwa kutibu.
Leaf mosaic virus, ugonjwa huu umezikumba pilipili zangu zilipoanza tu kutoa maua. Inasemekana hivi ni virus vinavyosambazwa na vipepeo wadogo weupe. Japo katika kukagua shamba langu sijawahi kuona vipepeo hivyo lakini inawezekana mimea hii ilipata ugonjwa huu ikiwa kitaluni kwani miche hii nilinunua na sikujua imetunzwaje. Dalili za ugonjwa huu ni majani kubadili rangi na kuwa mchanganyiko wa njano na kijani na baadaye hujikunja na kukauka kuanzia usawa wa ardhi kuja katika mashina. Mizizi hubaki mizima. Ugonjwa huu hauna tiba hivyo inashauriwa kung'oa mimea iliyoathirika na kuiteketeza ili kuzuia ugonjwa huu kuenea kwa mimea ambayo haijaathirika.

Maandalizi kilimo cha mboga (Chinese) 0.25 acre
Miche ya chinese ikiwa kwenye kitalu kabla ya kuhamishiwa shambani.
Uhamishaji wa miche ya chinese ukiendelea shambani.
Maua na matunda
Pilipili zimeanza kutoa maua na matunda ya mwanzo mwanzo. Wakati huu wa kutengeneza tunda ni muhimu sana mmea kupata maji ya kutosha na virutubisho muhimu. Hivyo ni wakati wa kuweka mbolea za majani (finishers boosters) mf Multi K.
Nyumba ya shambani
Watu wengi wanapenda kuita banda lakini kwangu mimi hii ni nyumba kabisa na kuna watu wanaishi nyumba za aina hii maisha yao yote.
Monday, December 5, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)