Hose Pipe 3" |
Sucking pipe (koromeo) |
Water pump BOSS WP80 |
Ili uweze kufanya kilimo chenye tija na cha kibiashara, ni lazima uchague zao ambalo litakupa faida nzuri zaidi kurudisha nguvu zako, muda wako na hata mtaji wako uliotumia. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye kilimo kwa sababu mbali mbali ikiwemo:-
- Mtaji - Kama ilivyo katika biashara nyingine pia katika kilimo bila kuwa na mtaji wa kutosha huwezi kufanya kilimo cha kibiashara ni lazima ujue zao lako kabla ya kuanza kulima litahitaji mtaji wa kiasi gani. Vinginevyo unaweza kuishia njiani na hivyo kupata hasara kubwa.
- Maarifa - Bila kuwa na maarifa sahihi juu ya zao unalotaka kulima ni rahisi kupata hasara. Ni lazima ujue ni mbegu gani nzuri, aina ya upandaji, maradhi, wadudu na muda wa kuweka mbolea na kipimo chake.
- Juhudi - Biashara hii ya kilimo hasa kilimo cha mboga mboga inahitaji usimamizi wa karibu. Ukiwa mzembe kwenye usimamizi ni rahisi kutokuvuna chochote au ukatumia gharama kubwa sana katika kukiendesha kutokana na wasamamizi utakaowaweka kutokuwa waaminifu. Ni vyema kabla hujaanza kulima kuhakikisha unao muda wa kuweza kusimamia shamba lako.
- Masoko - Endapo usipokuwa makini katika masoko, mambo yote niliyoeleza hapo juu yanaweza yasiwe na maana hata kama uliyatekeleza kwa asilimia mia moja. Unaweza ukapata mazao bora na ya kisasa lakini yakaozea shambani kwa kukosa soko na hivyo kupoteza mtaji na nguvu zako. Kabla hujaanza kulima lazima ujue soko la zao utakalolima pindi uvunapo. Ni lazima ufanye utafiti wa soko kwa kupata majibu ya maswali yafuatayo: Je ni wakati gani zao fulani linaadimika sokoni? Je hilo zao wateja wanapenda la aina gani, kama ni nyanya je wanapenda kubwa au ndogo ndogo au za wastani? Je gharama za uzalishaji ni ndogo kuliko faida kwa makadirio ya chini nayotegemea kupata? Ukipata majibu ya maswali hayo ndio uingie kuanza kulima huku ukijua muda utakaovuna mazao yako bei ya soko inatazamiwa kuwaje.
No comments:
Post a Comment