Tuesday, December 6, 2016

Magonjwa ya pilipili kali

Nimeona katika pilipili nazolima zinashambuliwa sana na ukungu. Hivyo ni vyema kupuliza dawa za kukinga ugonjwa huu kama Ebony 80WP au dawa za kutibu kama tayari zimeshaathirika, dawa kama Ivory 72WP ni nzuri kwa kutibu.




Leaf mosaic virus, ugonjwa huu umezikumba pilipili zangu zilipoanza tu kutoa maua. Inasemekana hivi ni virus vinavyosambazwa na vipepeo wadogo weupe. Japo katika kukagua shamba langu sijawahi kuona vipepeo hivyo lakini inawezekana mimea hii ilipata ugonjwa huu ikiwa kitaluni kwani miche hii nilinunua na sikujua imetunzwaje. Dalili za ugonjwa huu ni majani kubadili rangi na kuwa mchanganyiko wa njano na kijani na baadaye hujikunja na kukauka kuanzia usawa wa ardhi kuja katika mashina. Mizizi hubaki mizima. Ugonjwa huu hauna tiba hivyo inashauriwa kung'oa mimea iliyoathirika na kuiteketeza ili kuzuia ugonjwa huu kuenea kwa mimea ambayo haijaathirika.

No comments:

Post a Comment