Ili kupata mazao bora inabidi kuandaa shamba vizuri kwa kulisafisha na kuondoa mabaki yote ya mazao ya zamani na kuyachoma moto ili kuondoa mazalia ya wadudu kutoka katika mazao yaliyopita. Ni vyema kufanya kilimo cha mzunguko ili kuepuka wadudu kufanya makazi ya kudumu katika shamba lako. Kwa pilipili mbuzi ni vyema kuchagua shamba ambalo halijawahi kulimwa karibuni nyanya, tumbaku au viazi mviringo kwani wadudu wanaodhuru mazao haya wanadhuru pia pilipili mbuzi.
No comments:
Post a Comment